Sunday, June 17, 2012

IBADA YA EAGT - CITY CENTER HII LEO NA MCHUNGAJI KATUNZI.

Kanisa la Evangilistic Assemblies Of God Tanzania - City Center lililoko jijini Dar es Salaam chini ya Mchungaji kiongozi Frolian Katunzi limefanya Ibada zake katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Bandari ulioko Manispaa ya Temeke Maeneo ya Tandika.

Akihubiri katika ibada ya leo Mchungaji Katunzi amesema kuwa ili Wakristo waweze kuwa washindi katika majaribu yanayowatesa hawana budi budi kuwa na Maombi endelevu bila kuchoka ili waweze kumshinda adui shetani.

Amefafanua zaidi kuhusu Mkristo kuwa mvivu katika Maombi ni kujijengea Kaburi la moja kwa moja katika Maisha ya Kiroho na kimwili, akiwa amejaa Roho mtakatifu amewaasa Wakristo wavivu na wanaopenda Miujiza pasipo wao wenyewe kuomba kwa bidii kuachana haraka na tabia hiyo ili kuwa na hakika ya usalama wa  maisha yao ya kila siku.

Katika siku ya leo watu wengi wameshiriki katika maombi ya Mtu mmoja mmoja kanisa hapo kwa ajili ya kuvunja roho chafu za kuwafanya wakristo kuwa wavivu na wenye kupenda miujiza kwa haraka zaidi.

Picha ya chini: Mchungaji Katunzi akihubiri hii leo Kanisani katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Bandari.

 Picha ya Chini: Mchungaji Katunzi akifanya Maombi kwa Mtu mmoja mmoja hii leo Kanisani katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Bandari.
c
 Picha ya Chini:Mchungaji Katunzi akifafanua injili ya Kristo Yesu katika Ibada ya leo, Kanisani Chuo cha Utalii Bandari.
 Picha ya Chini: Mtumishi Timoth Limbu akifurahi na Mkewe baada ya Kubariki Mtoto wao hii leo na Baadaye Mchungaji Katunzi Kumpa jina la Ezekieli kutokana na Baba yake kuwa Kiongozi wa wimbo wa Mifupa katika kwaya ya Majestic iliyo chini ya Kanisa la EAGT City Center
 Picha ya chini:Mkurugenzi wa WWI Jimbo la Temeke Rachel Katunzi ambaye pia ni Mama Mchungaji Katunzi akitoa ufafanuzi juu ya Umoja wa Akina mama Jimboni hii leo ndani ya Kanisa la EAGT City Center.
 Picha ya Chini: Baadhi ya Watu waliohudhuria Ibada ya leo katika Maombi ya Ulinzi wakiombewa na Mchungaji kwa Jina la Yesu ili wapokee Nguvu ya Kuomba wenyewe na kutopenda kuombewa na kuwa wavivu wa Maombi.

No comments:

Post a Comment